Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Joshua Nassari amewapongeza wananchi wa kata ya Nampindi na Nyamihyolo kwakujitolea na kupendekeza maeneo kwaajili ya ujenzi wa Shule mbili za Sekondari za kata kupitia mradi wa SEQUIPT.
Pongezi hizo amezitoa mara baada ya kutembelea eneo la Kijiji cha Sunsi na Makwa kata ya Nampindi na Kata ya Nyamihyolo 14,Disemba 2021.
Mhe Nassari amesema kuwa Serikali imetambua uhitaji wa Shule za Sekondari katika Kata hizi mbili ili kupunguza watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu
‘Niwapongeze kwakujitolea maeneo,Watoto sasa hawataenda kusoma mbali’’Amesema Mhe.Nassari
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi.Changwa Mkwazu ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan kwakutoa kiasi cha Tsh.1, 200,000,000 kwaajili ya ujenzi wa Sekondari za Kata kupitia mradi wa SEQUIPT.
‘’Tunashukuru’’Amesema Bi.Mkwazu
Kwa hatua ingine Mhe.Nassari ametoa wito kwa vijana kujikita katika shughuli ambazo zitawainua kiuchumi na kuacha kuwategemezi katika familia ili kuleta maendeleo.
‘vijana ndio tegemezi la Taifa letu,tujikite katika shughuli mbalimbali ili kujikwamua katika umasikini’’Amesema Mhe.Nassari
Mbali na kutembelea maeneo yaliyopendekezwa ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata kupitia Mradi wa SEQUIPT pia Mhe.Nassari amekagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu madarasa katika Kijiji cha Karukekere .
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda