Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Ally Hapi amewataka wataalamu Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuweka utaratibu mzuri wa manunuzi wa vifaa vya ujenzi ili miradi ya ujenzi iende kwa Kasi.
Hayo ameyasema Januari21, 2022 alipofanya ziara ya kukagua miradi maendeleo ya ujenzi wa Vituo viwili vya Afya na mapokezi ya Vyumba 87 vya madarasa .
Mhe Hapi amesema kuwa kumekuwa na tabia ya kuchelewesha kupeleka vifaa katika maeneo ya ujenzi na hivyo kufanya ujenzi kutomalizika kwa wakati na kusababisha wananchi kukosa haki yao yakupata huduma maeneo jirani.
“vifaa vinapochelewa wananchi wanakosa kupata huduma bora zaidi kutokana na mradi kutokamilika kwa wakati”amesema Mhe Hapi
Aidha Mhe.Hapi amewataka wananchi wa Kata ya Iramba na Kata Jiriani kushirikiana katika kuangalia kazi ya ujenzi unavoendelea ili uweze kukamilika kwa wakati.
“Mradi huu ni wa wananchi lazima mfuatilie ili mtambue fedha zenu zinavotumika.”amesema Mhe Hapi
Naye Mchungaji Hosea mkazi wa kijiji cha Isanju amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwakutembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha afya Isanju .
“Tunaomba huu uwe utaratibu wa kufika mara kwa mara ili tupate maendeleo mengine zaidi”amesema Hosea
Aidha Hosea amesema kuwa Wananchi wa Isanju wanatambua juhudi za Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwakuleta maendeleo kwa wananchi.
“Tunashukuru na kuzipokea Juhudi zake’’amesema Hosea
Kwa Hatua ingine Mhe.Hapi amewataka wakuu wa Idara kuwajibika katika nafasi zao kwakusimamia miradi inayotekelezwa ili kuleta maendeleo kwa Wananchi pamoja na kusimamia Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mbali na kutembelea maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Isanju Pia Mhe Hapia amewapongeza uongozi wa Kata ya Hunyari kwa Kazi nzuri ya kusimamia ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Hunyari.
‘Nimeridhishiwa na hatua ya ujenzi,Niwapongeze viongozi na wananchi kwakushirikiana’’.amesema Mhe.Hapi
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ilipokea kiasi cha shilingi 250,000,000 zinazotokana na miamala ya simu kwaajili ujenzi wa kituo cha Afya Isanju Septemba 2021 na Shilingi 250,000,000 Januari,2022 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Hunyari.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda