Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu George Stanley Mbilinyi siku ya tarehe 11/4/2024 alifanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri ya Wilaya bunda, hususani katika Jimbo la Mwibara.
Ndugu Mbilinyi alitembelea na kukagua kituo cha Afya Isanju na kukagua jengo moja baada ya jingine, alimuagiza Mganga mfawidhi wa kituo kuhakikisha anasimamia usafi wa mazingira katika kituo hicho kwa kuhakikisha mazingira yote nje na ndani ya kituo yanakuwa masafi.
Pia alimuagiza Muhandisi wa Halmashauri kuhakikisha anafanya thathimini ya kiasi cha fedha zinazohitaji kwa ajili ya umaliziaji wa jengo la mama na motto, ili kuondoa adha ya kuharibika kwa saruji ambazo zipo stoo pamoja na vifaa vingine vya ujenzi.
Aidha, Ndugu Mbilinyi alitembelea na kukagua mradi wa ufugaji wa samaki na kilimo cha umwagiliaji uliopo katika kijiji cha Mchigondo Kata ya Igundu, ambapo aliweza kukagua maabara ya kutotoleshea mayai ya samaki, vizimba vya samaki vilivyopo ziwa Victoria, mabwawa ya kufugia samaki wazazi na vifaranga vya samaki.
Mkurugenzi Mtendaji alitembelea na kukagua ujenzi wa matundu ya manne ya vyoo katika shule ya msingi Bulomba, matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Bulendabufwe na matundu matano ya vyoo katika zahanati ya Sunsi, ambapo ujenzi upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji katika miradi hiyo, Pia alikagua ujenzi wa tanki la maji katika zahanati ya Sunsi, na ukamilishaji wa vyumba viwili katika zahanati ya Sunzi.
Ndugu Mbilinyi, aliwaagiza wasimamizi wote wa miradi kuhakikisha wanafuata taratibu, kanuni na sharia za manunuzi za vifaa vya ujenzi kupitia mfumo wa Nest, pia alimuagiza Muhandisi kuhakikisha anaitembelea miradi hiyo mara kwa mara na kuhakikisha inajengwa kwa kufuata viwango sahihi na kukamilika kwa wakati.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji aliongozana na timu ya wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda