Kamati ya usalama ya Wilaya ya Bunda ikiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Ndugu Salum Mtelela siku ya tarehe 26/7/2024 ilitembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, kwa upande wa Jimbo la Bunda.
Lengo la ziara hiyo, ni kuona namna maelekezo yaliyotolewa katika Halmashauri kama yametekelezwa na kufanyiwa kazi, ambapo walitembelea na kukagua ukamilishaji wa nyumba za watumishi zilizopo katika kituo cha afya Hunyari ambayo ni (3in1), mradi wa maji uliopo Sanzante, ambapo walitembelea na kukagua chanzo cha maji, mradi wa barabara kutoka Kiloleri hadi Nyabuzume yenye urefu wa Km 4.1, kiwanda cha Vijana Moto kilichopo Mariwanda kinachojishughulisha na uchanganyaji wa virutubishi kwenye unga, Pamoja na shule ya sekondari Mariwanda.
Ndugu Mtelela alimuagiza, Mhandisi wa TARURA wa Wilaya ya Bunda kuhakikisha anakamilisha barabara hiyo kwa wakati na kuhakikisha wanatengeneza mahali ambapo magari yataweza kugeuza mwishoni mwa barabara.
Kamati ya usalama, pia, ilimpongeza Meneja TANESCO wilaya kwa kutimiza ahadi ya kufikisha umeme katika shule ya sekondari Mariwanda kwa wakati, na kumtaka kuhakikisha, anafikisha umeme mapema katika kiwanda cha Vijana Moto kilichopo Mariwanda, ili kiwanda hicho kiweze kuendelea na shughuli za kuendesha mashine na kukua kiuchumi.
Kiwanda kinachomilkiwa na kikundi cha Vijana Moto-Mariwanda
Ukaguzi ndani ya kiwanda
Kamati pia, ilimuagiza Meneja RUWASA wa Wilaya kuhakikisha anaongeza kasi katika ukamilisha wa ujenzi wa vituo vya wananchi vya kuchotea maji (DPs), ili waweze kupata huduma ya maji safi na salama kwa ukaribu, maagizo hayo aliyatoa wakati walipotembelea na kukagua mradi wa maji uliopo Kijiji cha Bukama, Kata ya Nyamuswa.
Katika ziara hiyo waliongozana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu George S. Mbilinyi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda