Kamati ya huduma za uchumi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 29/1/2024 ilifanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Diwani wa Kata ya Hunyari, Mh. Sumera Mzumari, walitembelea shamba darasa la Muhogo lililopo katika kijiji cha Bulamba, Kata ya Butimba na kuona maendeleo ya zao hilo, pamoja na kupata taarifa fupi kuhusiana na shamba darasa hilo.
Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu Ombeni Padon alisema, yapo mashamba 19 ya Muhogo katika vijiji 11 vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambayo yapo chini ya mradi wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi yenye thamani ya shilingi Millioni 14 na laki 9.
Kamati ilitembelea na kukagua eneo la kiwanja kilichotolewa na Wanakijiji wa Mariwanda kwa ajili ya ujenzi wa shule ya awali na msingi, ambapo Wanakijiji hao waliomba wapate Mtaalamu wa kuwachorea mchoro ili waanze ujenzi kupitia nguvu za wananchi.
Kamati ilimuagiza Mhandisi wa Halmashauri kuhakikisha anawapimia eneo wananchi hao na kuwapa ramani ya namna ya ujenzi wa shule hiyo, ili waweze kuanza mapema ujenzi wa shule hiyo ya Awali na Msingi katika eneo hilo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda