• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANUFAIKA WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WASISITIZWA KUTUMIA FEDHA HIZO KUJIINUA KIUCHUMI

Posted on: December 31st, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imekabidhi hundi ya zaidi ya Tsh. milioni 180 kwa vikundi 34 vya wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu siku ya tarehe 31/12/2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Akizungumza na wanufaika wa mikopo hiyo wakati wa kukabidhi hundi,kaimu  Mkuu wa Wilaya ya Bunda  Mhe, Meja Edward Gowele ambaye pia alikuwa mgeni rasmi, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kutekeleza agizo la Mh. Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mikopo hiyo ya asilimia 10 itakayosaidia kuongeza mapato ya Halmashauri.

Aidha, amewasisitiza wanufaika wa mikopo hiyo kutumia vyema fedha hizo kwa kuzingatia  malengo ya kikundi  na kujenga  uchumi  wa Halmashauri na familia zao kama ilivyo azma ya serikali ya kuwainua wananchi kiuchumi.

.“Ni lazima kurejesha fedha hizo kama kikundi na uaminifu utawasaidia kuendelea kupata mikopo zaidi na kutoa fursa kwa vikundi vingine ambavyo havijakidhi vigezo vya kupata mikopo hii, ili kuweza kupewa mikopo hiyo kwa  awamu nyingine.” Amesema Mhe.Gowele

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw. George S.Mbilinyi amewataka wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 kutumia fedha hizo kuwanufaisha katika biashara zao na kuwainua kiuchumi huku akiwasisitiza kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.

“Dawa ya mkopo ni kulipa hakikisheni mnalipa kwa wakati mikopo hiyo ilikuweza kupata nafasi ya kupata mikopo zaidi.”amesema Mbilinyi

Nao baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo ya asilimia 10 wameishukuru serikali ya awamu ya sita (6) kwa kutoa mikopo hiyo na kuahidi kutumia fedha hizo kujiinua kiuchumi kwa kufanya biashara zenye tija ili kuweza kurejesha mikopo hiyo kwa wakati sahihi.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA MPANGO MKAKATI

    April 25, 2025
  • PROJECT ZAWADI YAIPIGA TAFU MASHINDANO YA UMITASHUMTA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

    April 07, 2025
  • WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA TUZO NA ZAWADI .

    April 03, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika: 0742163056

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda