Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Musoma Vicent Naano amewataka wadau wa uwekezaji wilaya ya Bunda kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwl. Lydia Bupilipili kuhakikisha wanaunda kamati ya kimkakati ya kufuatilia maswala ya uwekezaji.
Mhe. Naano alitoa kauli hiyo Juni 15,2021 kwenye kongamano la uwekezaji ambalo limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda kwa kushirikiana na wadau wa uwekezaji lililofanyika Katika Chuo cha Ualimu Bunda.
Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi kuhusu kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili alisema Wilaya ya Bunda imejaliwa kuwa na vivutio vingi hivyo ameamua kuja na mpango mkakati wa kutambua vivutio hivyo huku akiwaalika wawekezaji kuja kuwekeza Wilaya ya Bunda.
Mhe.Bupilipili alitaja baadhi ya fursa hizo kuwa ni hotel za kitalii,michezo ya ziwani,Kupanda Mlima Balili na Chamriho ambayo wageni wanaweza kuona Hifadhi ya Taifa Serengeti ba Fukwe za Ziwa Viktoria.
“Bonasi ya kuwaona wanyama kabla hujalipia inapatikana Bunda pekee,njooni mjenge hotei za kitalii ,mtu anayetaka kutalii,aogelee hadi achoke,aje Bunda au atembelee Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa urahisi,au apande mlima atakaoona ziwa na wanyama kwa wakati mmoja,aje hapa Bunda’’alise mhe Bupilipili
‘’Maeneo ya kuwekeza yamejaa na usalama upo wa kutosha,yeyote atakayeonesha kuwa anataka kuwekeza Bunda katika sekta yeyote tutamlinda’’alisisitiza Mhe Bupilipili
Awali,akifungua kongamano hilo Mhe. Vicent Naano alisema kwamba licha ya eneo kubwa la Hifadhi ya Serengeti lipo licha ya eneo kubwa la Hifadhi ya Serengeti lipo mkoani Mara,wakazi wake hawajachangamkia ili kuwanufaisha hiyo,kama ambavyo mikoa mingine ya Arusha na Kilimanjaro inanufaika.
“Huu mkoa ulikuwa umefungwa,yaani watalii wakija hawashukii hapa,kuitafuta TANAPA hadi uwende Arusha,unakuta Wilaya kama TARIME ipo mpakani watalii wanapita tu,sasa tumieni fursa zilizofunguliwa kuutajirisha mkoa huu’’alisema Mhe.Naano
Aidha Mhe. Naano ameitaka Wilaya ya Bunda kuhakikisha inaunda kamati itakayofuatilia masuala yote ya utalii na uwekezaji,ambayo itakuwa inakutana kila baada ya miezi miwili,chini ya katibu Tawala Mkoa(RAS) wa Mara.
Naye afisa wa uhifadhi endelevu na utunzaji wa Mazingira WWF bwana Kanuni Kanuni amesema kuwa WWF imekua ikifanya utunzaji wa Mazingira na kuhifadhi wanyamapori ili kuhamashisha wawekezaji ndani ya mkoa wa Mara
Kwa upande wake muwakilishi wa Serengeti safari Marathon ambaye pia ni mkurugenzi wa NCT twende kutalii Albert Chenza amesema wao kama wadau wa utalii wako tayari kushirikiana na serikali katika kukuza uwekezaji wa utalii ndani ya wilaya ya Bunda katika vivutio vyote vilivyo ainishwa.
Kongamano la uwekezaji na fursa za utalii lilihudhuria na viongozi mbalimbali wa kiserikali, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya,Waheshimiwa Madiwani na viongozi wa Dini,Wafanyabiashara,wananchi na wazee maarufu
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda