Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Joshua Nassari amezitaka Jumuiya za watumiaji maji Wilaya ya Bunda kusimamia ipasavyo miradi ya maji iliyo katika maeneo yao, kwa kuhakikisha kuwa fedha zinazokusanywa zinatumika vizuri ikiwemo na kulipia bili ya maji kila Mwezi.
Hayo amesema leo Oktoba 7,2021 katika Mkutano wa kwanza wa Wadau wa Sekta ya Maji Wilaya ya Bunda uliosimamiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijiji(RUWASA) uliofanyika katika ukumbi wa Malaika uliopo Bunda Mjini.
‘’Sisi kama wadau ,kama viongozi ni lazima tuhimize wananchi walipie huduma ya maji ili kuepusha usumbufu wakukatiwa maji’’amesema Nassari
Aidha Mhe Nassari amesema kuwa fedha zote zinazokusanywa na jumuiya ya maji kutoka kwa Wananchi wa eneo husika zinatakiwa kubaki ili kutanua mtandao wa maji katika maeneo hayo sambamba na hilo kuhakikisha miundombinu inatunzwa na kuthaminiwa ili kuepusha manunuzi na marekebisho ya miundombinu.
‘’serikali inahakikisha kuwa kila mwananchi anafunga maji nyumbani,katika juhudi za kupambana Kumtua ndoo mama kichwani’’amesema Mhe.Nassari
Naye,muwakilishi wa meneja wa RUWASA mkoa wa Mara afisa utumishi Stanley Sing’ira amebainisha kuwa lengo la RUWASA ni kuhakikisha Mamlaka hiyo inatoa huduma ya maji kwa wananchi huku akiendelea kusisitiza jumuiya za maji kuendelea kusimamia miradi ya maji ili iwe endelevu.
‘’Maji ni muhimu katika shughuli zetu za kila siku ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha maji yanapatikana kwa kila mwananchi na kwa wakati’’amesema Sing’ira
Kwa upande wake meneja wa RUWASA wilaya ya Bunda Eng. Lukas Madaha amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu vya kuhujumu miundombinu ya maji kwani kwakufanya hivyo ni kinyume na taratibu za sheria na atakae bainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.
‘’kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kuharibu pamoja nakuchukua vifaa na kupelekea huduma katika eneo husika kupotea,hivyo niwaombea wadau tuwasisitize wananchi kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake katika kulinda miundombinu ya maji’amesema Eng. Madaha
Mkutano huo uliambatana na mada mbalimbali zikiwemo Mada migogoro katika kamati za maji,utaratibu wakuunda vyombo vya watumiaji maji ngazi ya jamii na uendeshaji wake,programmu nzima ya Maji na Upangaji bei maji.Sambamba na mada zilizotolewa aidha wajumbe walipata nafasi ya kujadili na kupata maazimio ya mkutano wa kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Maji.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda