Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Dkt Vicent Anney, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya nyumba sita za walimu wa shule ya msingi Busore, iliyopo kijiji cha Bukama, Kata ya Nyamuswa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Hafla ya makabidhiano ya nyumba hizo yaliyafika siku ya tarehe 23/8/2024 katika viwanja vya shule ya msingi Busore, ambapo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda alizindua na kuzikabidhi kwa walimu wa shule ya msingi Busore.
Mh. Dkt Anney aliwashukuru shirika la Project Zawadi wakiwa ni wadau wakubwa wa maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda hasa tarafa ya Chamriho kwa upande wa elimu, wamekuwa wakitoa elimu kuhusiana na masuala ya lishe bora kwa shule zilizopo Kata ya Nyamuswa, wamekuwa ni wadau wa maendeleo kwa upande wa miradi ya maji, na umeme.
“Tunawashukuru sana shirika la Project Zawadi kwa kutujengea nyumba hizi nzuri na za kisasa, ambazo zina miundombinu yote muhimu kama maji na umeme, tunapenda kuwashukuru sana kwa kuendelea kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha tunaboresha elimu kwa wanafunzi kwa kuhakikisha walimu wanaishi kwenye makazi bora.” Alisema Dkt Anney.
Meneja Program ya Ufadhili wa Wanafunzi, kutoka shirika la Project Zawadi Bi. Regina Mkama alisema ujenzi wa nyumba hizi ulianza tarehe 2/3/2021 na kukamilika tareheb31/7/2024 lengo kuu likiwa ni kuboresha mazingira mazuri ya kuishi walimu katika shule ya msingi Busore na kuwapunguzia kero wanazopitia walimu za kutafuta makazi ya kuishi nje ya eneo la shule. Kero hizo huchangia kuzorotesha juhudi za kutoa elimu bora kwa wanafunzi.
“Hadi kukamilika kwa mradi huu wa ujenzi wa nyumba sita za walimu, jumla ya Tshs Million 176,192,736 zimetumika, ambapo kiasi cha Tshs Million 161,612,736 zilitolewa na shirika la Project Zawadi na kiasi cha Tshs 14,580,000 ni michango ya wananchi kupitia nguvu zao zikihusisha uletaji wa viashiria vya ujenzi ambavyo ni kokoto, udongo, mchanga, mawe na maji.” Alisema Bi. Mkama.
Shirika la Project Zawadi linatekeleza miradi ya elimu katika shule 46 katika vijiji 28 kwenye Kata 7 ambazo ni, Nyamuswa, Ketare, Mihingo, Mugeta, Nyamang’uta, Hunyari na Salama.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda