Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara imeandaa tamasha la Nyamachoma lijulikanalo kama Nyama choma Festival, litakalo fanyika katika stend ya zamani iliyopo Bunda Mjini siku ya tarehe 8/11/2024.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Dr. Vicent Anney amesema, tamasha hilo litawahusisha wananchi wote wa wilaya Bunda na maeneo ya jirani huku lengo kuu likiwa ni kuhamasisha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unao tarajia kufanyika tarehe 27/11/2024.
“Tumeandaa tamasha hili mahususi ilituweze kukutana na wananchi wote wa Wilaya ya Bunda kwa ajili ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajia kufanyika mwezi kumi na moja tarehe 27, 2024 ili kila mwananchi aweze kufahamu haki yake ya kikatiba katika kupiga kura na kuweza kuchagua viongozi walio bora na sahihi ambao watashirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kijiji na kitongoji. Amesema Mh. Dkt Anney.
Ameongeza kuwa, wananchi wengi bado hawana hamasa ya kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa hii nikutokana na ukosefu wa elimu juu ya umuhimu na faida za kushiriki uchaguzi hususani wa serikali za mitaa katika kuchagua viongozi wa kjiji, vitongoji, na wajumbe wa halmashauri ya kijiji.
“Watu wengi bado wanadhana ya kufikiri kuwa zoezi la uchaguzi ni mahususi kwa baadhi ya makundi ya watu pasipokufahamu kuwa zoezi la uchaguzi ni haki ya kila Mtanzania aliyetimiza vigezo vya kushiriki zoezi hilo” Amesema Mkuu wa Wilaya.
Aidha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tamasha la Nyamachoma Festival ambalo linahusisha mambo mbalimbali ikiwemo michezo na ngoma za asili na zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi wa watakao choma nyama vizuri, tamu na yenye ladha.
Uchaguzi wa serikali za mitaa una husisha kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea kwenda kupiga kura na kumchagua kiongozi mwenye sifa sahihi, na kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 21 na kuendelea anayohaki ya kugombea nafasi ya uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na ni lazima awe amejiandikisha kwenye daftari la mpiga kura la serikali za mitaa.
Seikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda