Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipi amewataka Viongozi wa Ngazi ya Kata na Vijiji kuhamasisha Wazazi na Jamii nzima kwa ujumla kuhusu lishe bora na chakula mashuleni ili watoto waweze kumudu masomo.
Hayo yamesememwa Mei 18,2021 katika Ukumbi wa Halmashauri wakati wa kupokea Tathimini ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi,2021.
Mhe Bupilii alisema kuwa Serikali imetambua umuhimu wa afua za lishe nchini na imetoa msukumo zaidi kuimarisha afya kwa kufunga mikataba kuanzia Ngazi ya Mkoa mpaka ya Kata.
‘Sisi kama viongozi hatuwezi kulibeza swala la lishe katika jamii’’.alisema Mhe Bupilipili
Mhe Bupiliupili alitoa wito kwa watendaji wa Kata kuendelea kujitolea kuhamisisha wananchi kuhusu Lishe bora hasa mashuleni.
‘’Tunaeza walaumu kuwa walimu hawajafundisha vizuri watoto wamefeli,wakati mtoto hapati lishe iliyobora ikamfanya akatulia na kumsikiliza mwalimu’’alisema Mhe Bupilipili
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri Dkt Nuru Yunge alisema kuwa utekelezaji wa viashiria vya Mkataba wa Afya umekuwa hautekelezwi kwa ufanisi katika Halmashauri kama ilivyopangwa kutokana na changamoto kubwa zaidi ni ukosekanaji wa fedha .
‘’Mimi Mganga Mkuu,kushirikiana na Afisa Mipango na Wataalam wengine tuweze kuandika maandika mbalimbali ambayo yatatusaidia kupata fedha ambayo itatusaidia kutekeleza afua za lishe ilikuboresha afya za jamii katika Halmashauri yetu’’Alisema Dkt Yunge
Dkt Yunge alisema kuwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wana nafasi kubwa ya kupata lishe bora kutokana na Mazingira yao wanaoishi.
‘’Jamii isifikirie lishe bora ni kula nyama ya kuku,unaeza ukalima mboga za majani na mazao mengine kwa gharama nafuu na ukapata mchanganyo wa lishe bora’’Alisema Dkt Yunge
Naye, Bi Magreth Arbogast kwa niaba ya Afisa Lishe alitaja madhara wanayoweza kutokea mtu anapokosea lishe bora ni Utapiamlo,na kwa wajawazito anaechelewa kuanza kliniki ni pamoja na kuzaa watoto wenye matatizo ya mgongo wazi,mdomo sungura na kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa.
Aidha Bi mage amezitaka jamii kuzingatia lishe bora pamoja na kuzalisha vyakula vyenye virutubisho kwa wingi kama viazi lishe,maboga,mboga za majani na mazao mengine.
‘’kila mwanajamii aone umuhimu wa kuwepo wa mazao yatakayomsaidia kupata lishe bora’alisema Bi Arbogast
Kwa hatua ingine Dkt Yunge aliwashukuru wadau wa lishe ambao ni PCI,Kizazi Kipya,Americares na USAID Boresha Afya kwa kuwajengea uwezo wahudumu wa Afya kwa ngazi ya jamii.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda