• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKUU WA WILAYA YA BUNDA AFANYA MKUTANO WA HADHARA WANAKIJIJI ,KARUKEKERE

Posted on: October 24th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Dr. Vicent Anney amefanya mkutano wa hadhara na Wanakijiji cha Karukekere, Kata ya Namuhula katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kusikiliza kero na changamoto wanazokabiliana nazo.

Mkuu wa Wilaya alikutana na Wanakijiji hao alipokuwa akifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali katika Kijiji hicho siku ya tarehe 23/10/2023.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Karukekere Bw. Daniel Peter Ngawa, alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuja kuwatembelea na kukagua miradi mbalimbali waliyonayo katika Kijiji chao, pia alimueleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo miundombinu ya Barabara kutokuwa rafiki hasa  wakati wa mvua, njia kushindwa kupitika kutokana na ubovu wa Barabara na kukatika kwa madaraja, hivyo kupelekea shughuli  nyingi za kiuchumi kukwama.

Bw. Ngawa alisema mbali na changamoto wanazokabiliana nazo, Kijiji kimeweza kuchangia kiasi cha Tshs Milioni 20 ya mapato yao katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kutokana na zao la Dengu kwa mwaka 2023.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alianza kwa kusema, changamoto kubwa aliyoiona ni wananchi wengi kutokuwa na vyoo, hivyo alimuagiza Mtendaji wa Kijiji pamoja na vitongoji kushirikiana kwa pamoja katika kusimamia masuala ya uchimbaji wa vyoo katika kaya ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa.

Alimuagiza Mtendaji wa Kijiji kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 30/10/2023 ahakikishe wanapita kwenye kila kaya na kukagua watu wasiokuwa na vyoo na kuanza kuwachukulia hatua ikiwemo kuwatoza faini.

Mh. Dr. Anney alisema, changamoto nyingine aliyoiona kwenye Kijiji chao ni Watoto wengi kutokupelekwa shuleni hadi umri wa kuanza shule kupita, hivyo alimuagiza Mtendaji wa Kijiji kuhakikisha wanashirikiana na viongozi waliopo kwenye vitongoji kwa kupata takwimu sahihi na kuandikisha Watoto wote walio na umri wa kupelekwa shule lakini wapo nyumbani wahakikishe wanahudhuria shuleni na kuanza masomo mara moja.

Mkuu wa Wilaya alisema, suala la Barabara ameshamuagiza Meneja TARURA kuhakikisha anatatua changamoto hizo ili kuhakikisha barabara zinapitika kipindi chote kwa mwaka mzima. Pia alimuagiza Meneja TANESCO kuhakikisha wanaweka kwenye bajeti yao ya mwaka huu suala la kuwaletea umeme  Wanakijiji pamoja na  eneo la Mradi wa Maji ambao unatumia jenereta katika shughuli zake hivo kupelekea gharama za uzalishaji kuwa kubwa mno.

Mh. Dr. Anney aliwapongeza Wanakijiji na Viongozi wa Chama kwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi vizuri kwa kuhakikisha suala la elimu katika Kijiji chao wanalipa kipaumbele katika Ujenzi wa shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya kuhakikisha Watoto wao wanapata elimu iliyo bora na ya uhakika.

Pia aliwapongeza kwa Ujenzi wa Jengo la kinamama la kujifungulia katika Zahanati ya Karukekere walilolijenga kwa nguvu ya wananchi, hivyo aliwaahidi kuwachangia kiasi cha Tshs Milioni Moja ili kukamilisha Ujenzi huo.

Mkuu wa Wilaya aliwaagiza Wanakijiji kwa mwaka huu kuhakikisha wanapanda zao la Mtama na Pamba kwa ajili ya kujiongezea mapato katika Kijiji chao, na kuwaasa kuacha tabia ya kuchanganya zao la Pamba na Mahindi katika shamba moja kwani ni hatari sana, hii ni kutokana na dawa zinazopuliziwa kwenye Pamba kuwa ni kali na hatari kwa Afya ndio maana aliwaasa kuacha tabia ya kuchanganya mazao hayo pamoja wakati wa upandaji.



Mh. Dr. Anney alimuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw. Oscar Jeremiah Nchemwa, kuhakikisha mbolea inaletwa katika Kijiji chao. Pia aliwaomba Wanakijiji kutunza Ulinzi na usalama.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA MPANGO MKAKATI

    April 25, 2025
  • PROJECT ZAWADI YAIPIGA TAFU MASHINDANO YA UMITASHUMTA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

    April 07, 2025
  • WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA TUZO NA ZAWADI .

    April 03, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika: 0742163056

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda