Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh. Said M. Mtanda siku ya tarehe 4/1/2024 amefanya mkutano na Wakandarasi wote wanaojenga katika shule ya sekondari ya Mkoa ya wasichana, iliyopo katika kijiji cha Bulamba, kata ya Butimba, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Mbali na mkutano huo Mh. Mkuu wa Mkoa alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo, kwa kukagua jengo moja baada ya lingine, ili kuona maendeleo ya mradi huo ulipofikia.
Mh. Mtanda aliwaambia wakandarasi hao lengo la ziara yake ni kwaajili ya kuona maendeleo ya mradi huo wa ujenzi ulipofikia, na kuwasisitiza kuongeza kasi zaidi katika kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati.
Pia, aliwaambia anatarajia kuja kuupokea mradi huo mwishoni mwa mwezi wa Kwanza hivyo aliwataka wakandarasi wote kuhakikisha wanaukabidhi mradi kwa tarehe husika.
“Tunataka Wakandarasi waadilifu katika mradi huu ambao wanafanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati. Mradi kama huu unatekelezwa Kitaifa katika mikoa 16 na Halmashauri hii ni mojawapo katika kutekeleza mradi huu wa ujenzi wa shule ya Mkoa ya wasichana, hasahasa katika Kijiji hiki cha Bulamba, Kata ya Butimba, Tuishukuru serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha kutupatia kiasi cha Tshs Bilion 4 katika mradi huu.” Alisema Mh. Mtanda.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliwaambia hatamvumilia mtu yeyote yule mwenye nia ya kuhujumu mradi huu, hivyo aliwataka kufanya kazi kwa uadilifu na kwa uaminifu ili kuhakikisha mradi unakamilika na kuukabidhi kwa wakati sahihi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda