Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 8/2/2024 ilifanya mkutano wa baraza la wafanyakazi, na lengo kuu la mkutano ilikuwa, ni kujadili mpango na bajeti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, uliopo eneo la Kibara Stoo, na ulihudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Wawakilishi wa chama cha wafanyakazi (TAWLGU), wawakilishi Chama cha Walimu (CWT) na Wawakilishi wa chama cha wafanyakazi (TUGHE).
Wajumbe wa baraza walijadili bajeti hiyo kwa kupitia kurasa kwa kurasa, na palipojitokeza mapungufu walitaka yarekebishwe.
Wajumbe waliwashauri watumishi kupendana na kushirikiana kwa pamoja katika utendaji wao wa kazi, pia walisisitiza suala la kuheshimiana watumishi wote na kila mmoja kuhakikisha anawajibika katika utendaji wake wa kazi, ili kuleta usawa pasipo kupendelea upande wowote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi. Changwa M. Mkwazu aliwashukuru Wajumbe wote kwa ushirikiano wao na michango yote waliyoitoa na kuwaahidi kwenda kuyafanyia kazi na kuhakikisha wanarekebisha pale walipokosea.
“Niwaombe wajumbe tuendelee kushirikiana kwa pamoja, na kuthaminiana watumishi wote.” Alisema Bi. Mkwazu.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda