Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh.Dkt Vincent Anney siku ya tarehe 27/1/2025 alifanya kikao na wafanyabiashara wa Wilaya ya Bunda akiwa na lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika sekta ya kilimo,uvuvi,miundombinu,maji na kimfumo.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndugu Salum Khalfan Mtelela aliwakaribisha na kuwashukuru wafanyabiashara wote waliohudhuria katika kikao hicho na kuwaeleza mbali na kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali wanazopitia, pia, kuangalia fursa za kibiashara zilizopo katika Wilaya ya Bunda na kuona ni kwanamna gani wananchi wote wanaweza kunufaika na fursa hizo kupitia sekta mbalimbali zilizopo na kuona ni namna gani wataweza kuziboresha ili wananchi waweze kunufaika nazo.
Katika kikao hicho mbali na wafanyabiashara kuhudhuria pia walikuwepo madiwani wote wa Halmashauri ya zote mbili, Wakurugenzi watendaji, kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, wakuu wa taasisi mbalimbali zilizopo Wilaya ya Bunda pamoja na wakuu wa vitengo na divisheni kutoka Halmashauri zote mbili za Bunda Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Ndugu Mtelela alisema, nimewaalika wote hapa ili kuweza kutolea ufafanuzi yale yote ambayo yatahitajika kutoka kwa wafanyabiashara ikiwemo kufahamiana na kujenga mahusiano mazuri baina yenu wote.
Wafanyabiashara waliweza kueleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo masuala ya kutumia mfumo, kupishana kwa sera za serikali katika kubainisha mipaka yao kati ya serikali kuu na serikali za mitaa na kata katika masuala ya ulipaji wa ushuru wa serikali na usumbufu wa kudaiwa kodi za Halmashauri na TRA.
Wafanyabiashara waliomba serikali iwaboreshee mazingira mazuri ya yakufanya biashara zao katika sekta za ufugaji, kilimo,uvuvi na miundombinu.
Pia, waliomba walipwe madeni yao wanayozidai Halmashauri zote mbili ili waweze kuendelea na biashara zao kutokana na kuwahudumia katika kuwasambazia vifaa mbalimbali katika Halmashauri hizo.
Ndugu Mtelela aliwaahidi wafanyabiashara changamoto zote pamoja na maombi yao wataenda kuyafanyia kazi na kuhakikisha yanatekelezwa kwa wakati ikiwemo ulipaji wa madeni wanayodai kwa Halmashauri.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda