Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipili ameawagiza Madiwa wa Halmashuri ya Wilaya ya Bunda kufuatilia na kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kila kata na Kijiji.
Hayo yamesemwa Disemba 16, 2020 wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa kanisa uliopo Kibara.
Mhe Bupilipili amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi kuendeleea kushirikiana na wananchi katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili wananchi waweze kuchangia nguvu zao katika kukamalisha miradi ya maendeleo
“wananchi wanaposhirikishwa wanakuwa walinzi wa mradi husika”.alisema Mhe Bupilipili
Pia Mhe Bupilipili amewaagiza Madiwani kuendelea kusimamia mapato Kwakuanzisha kilimo cha mseto,kutangaza utalii pamoja nakuendelea kuhamasisha wananchi kuendelea kulima zao la pamba
“Endapo madiwani mtasimamia na kuzingatia ninaimani mapato ya halmashauri ya taongezeka huku itasaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na nguvu za Wananchi”.alisema Bupilipili.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda Mhe Charles Manumbu amewashukuru Madiwani kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Bunda kwa kipindi cha miaka Mitano na kueleza kwamba atatoa ushirikiano mkubwa katika kuliongoza Baraza la madiwani ilikuleta tija na manufaa kwa Wananchi pamoja na Halmashauri.
“Binafsi nitaongoza baraza hili kwakufuata kanuni ,taratibu pamoja na miongozo iliyowekwa ili kuweza kuleta manufaa kwa sasa na kizazi cha baadae”.alisema Mhe Manumbu
Aidha Mhe Manumbu amewataka Madiwani hao kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa watumishi.
Kwa upande wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda , Bwa.Amos Kusaja amewasilisha taarifa ya shughuli za Serikali zilizotekelezwa na Watumishi kwa kipindi cha kuanzia mwezi Mei hadi Novemba 2020,nakueleza kwamba shughuli hizo zimetekelezwa na Menejimenti ya Halmashauri ambapo utekeleza wa miradi na shughuli nyingine umefanyika katika Idara na Vitengo na Sekta Zote.
Ramadhani Dallo Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda amesisitiza ushirikiano mzuri baina ya Watumishi na Madiwani ili kuweza kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa uwadilifu kwa maslahi ya Wananchi na kuifanya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda isonge mbele isirudi nyuma.
“Ni jambo jema sana kushirikiana na kufanya kazi kwa upamoja ili tusonge mbele”.Alisema Dallo
Aidha Dallo ametoa wito kwa Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha madiwani wanafahamu stahiki zao na stahili na kutimizwa pindi panapo stahili ili kuepusha mgawanyiko .
“Mkurugenzi hakikisha madiwani wanapata kufahamu stahiki zao ili wapate nafasi yakufanya kazi vizuri.”alisema Dallo
Jumla ya Madiwani 25 walikula kiapo na kati ya hao 22 ni wachama cha Mapinduzi(CCM),2 ni CHADEMA na mmoja kutoka ACT.
Kikao hicho pia Kilihudhuriwa na Katibu tawala Wilaya,Viongozi wa Taasisi mbalimbali ,Afisa Uchunguzi na Wananchi.
Mwisho.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda