Shirika la Project zawadi ambao ni wadau wakuu wa maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 5/4/2025 walitoa msaada wa vifaa mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Msaada huo walikabidhi kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Oscar Jeremiah Nchemwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo, ambapo shirika lilikabidhi katoni kadhaa za maji ya kunywa, dawa za kuchua misuli, pamoja na glucose kwa ajili ya washiriki wa mashindano ya UMITASHUMTA.
Ndugu Nchemwa aliwashukuru shirika la Project zawadi kwa msaada mkubwa walioutoa kwa ajili ya kuwasaidia washiriki wa mashindano hayo ambapo mashindano yalishirikisha wanafunzi kutoka tarafa zote tatu zilizopo katika Halmashauri, ambazo ni tarafa ya Nansimo, Chamriho na Kenkyombo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda