Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Mashimba Ndaki amewataka wafugaji kuhakikisha wanafuata taratibu za ufugaji ili kuepusha mifugo kupata magonjwa.
Hayo amesema Disemba11, 2021 alipotembelea na kuzindua Josho katika kijiji cha Sarakwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Mhe Mashimba amesema kuwa kila mfugaji aone umuhimu wa kuogesha mifugo pamoja na kuchanja ili kuepusha magonjwa kwa mifugo pamoja na kuwafanya wawe na afya nzuri.
"Aslimia 95 ya magonjwa hutokana na kutofuata utaratibu wa ufugaji,hivyo kila mfugaji aone umuhimu wa kuzingatia taratibu za ufugaji" amesema Mhe.Ndaki
Aidha, Mhe.Ndaki ameeleza kuwa Wizara imeweka mpango mkakati wa kampeni ya kupanda malisho kwa wafugaji ili mifugo isipate changamoto wakati wa kiangazi
‘’Kampeni hii itasaidia mifugo yetu kupata malisho wakati wote", aliongeza Mhe. Ndaki
Awali akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa josho mpaka kukamilika, Mjumbe wa Serikali ya kijiji Bi.Barenda Kitasha amesema kuwa ujenzi ulianza 22.7.2021 na mpaka kukamilika gharama zilizotumika ni kiasi Tsh.25,150000 ikiwa Milioni 18 kutoka wizara ya mifugo na Uvuvi na Tsh.7,150,000m ni nguvu kazi za Wananchi pamoja na Wadau wengine.
Bi.Kitasha amesema kuwa ujenzi umetekelezwa kwakuzingatia sheria na taratibu zote za ujenzi,viwango stahiki vya ubora na usalama wa mifugo.
Katika hatua nyingine, Mhe.Mashimba ametoa wito kwa Halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo.
"Maeneo yote ya marisho yabainishwe na taarifa zipelekwe Wizarani’’, amesema Mhe.Ndaki
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mhe.Joshua Nassari amemshukuru Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa ujio wake Bunda, sambamba na kuhakikisha wafugaji Bunda wanapata ruzuku ya dawa kutoka Wizarani
‘’Naimani ujio huu utazaa matunda zaidi kwa wafugaji wa Bunda,Tunashukuru’’,amesema Mhe.Nassari
Mbali na uzinduzi wa Josho kijiji cha Sarakwa Mhe.Ndaki ametembelea Josho katika kijiji cha Kihumbu,Josho katika kijiji cha Mekomariro na Lambo la kunyweshea Mifugo katika Kijiji cha Salama kati.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda