Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Ally Hapi amewataka Madiwani pamoja na wataalam kushirikiana kwa pamoja katika kusimamia Miradi ya maendeleo inayotekelezwa ili kufanikisha lengo la Serikali kutatua changamoto kwa waananchi,
Hayo amesema leo Novemba 30,2021 baada ya kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne katika Shule ya Sekondari Makongoro na Ujenzi wa vyumba viwili katika shule ya Msingi Shikizi Suguti zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Mhe Hapi amesema kuwa kuna umuhimu wa kila kiongozi kuwajibika kwa nafasi yake pamoja na kushirikiana ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na viwango.
‘Msikae ofisini,muende maeneo ya mradi ili mkawasimamie mafundi vizuri,miradi ikamilike kwa wakati na viwango’.Amesema Mhe Hapi
Aidha Mhe Hapi amewataka viongozi kutojiingiza katika vitendo vya rushwa kwa kutaka kupata tenda katika maeneo ya miradi kwani kanuni za utumishi haziruhusu.
‘kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi kutaka kupata tenda ya kusambaza vifaa katika maeneo ya miradi,ukifanya hivyo utaingia katika maslahi binafsi ni vyema ukaacha’’amesema Mhe Hapi
Mhe Hapi ametoa wito kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuwajengea uwezo vikundi vya Wanawake,Vijana na Watuwenyeulemavu ili waweze kuanzisha miradi ya vifaa vya ujenzi.
‘Tukiviwezesha vikundi hivi Halmashauri pia itanufaika hasa katika miradi ya ujenzi’amesema Mhe.Hapi
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Joshua Nassari amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutembelea Wilaya ya Bunda na kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Mhe Nassari ameahidi kushirikiana na wakurugenzi wa halmashauri zote mbili ili kuhakikisha miradi inamalizika kwa wakati na Viwango.
‘Tunashukuru kwa Ujio wako Mhe Mkuu wa Mkoa,na niahidi tu sikuingine ukija utakuta miradi iko vizuri zaidi’’amesema Mhe Nassari
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi.Changwa .Mkwazu awali akitoa taarifa ya ujenzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa amesema kuwa changamoto ambayo imefanya kuchelewa kuanza ujenzi ni kuchelewa kupatikana kwa vifaa ikiwa pamoja na vifaa kuchelewa kufika kwenye maeneo husika kutokana na changamoto ya barabara.
‘Kumekuwa na changamoto ya vifaa hasa sementi,tunashukuru juhudi zimefanyika tumeanza kupeleka sementi katika maeneo mengi ya miradi’’Amesema Bi Mkwazu
Kwa hatua ingine Mhe.Hapi amesisitiza utulivu katika Mabaraza ya Madiwani kwakuhakikisha busara na hekima ina kuwepo katika kufanya maamuzi kwa masilahi ya Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ilipokea fedha za mpango wa maendeleo kiasi chaTshs. 2,550,000,000 fedha kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa 67, ujenzi wa jengo la huduma za dharura,ujenzi wa jengo la ICU na Nyumba za Watumishi .
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda