Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ambaye ni diwani wa kata ya Iramba Mh. Charles Manumbu siku ya tarehe 28/1/2025 aliongoza wajumbe wa kamati ya fedha, uongozi na Mipango kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kamati ikiongozwa na wakuu wa idara na vitengo walitembelea na kukagua ukamilishaji wa bwalo la chakula katika shule ya Sekondari ya wasichana Mara, ukamilishaji wa bweni Moja la wasichana, pamoja na ujenzi wa mabweni manne ya wasichana na Madarasa pamoja na majengo mengine yanayajengwa katika shule hiyo ya Sekondari ya wasichana Mara.
Pia, kamati ilitembelea na kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari iliyopo Kijiji cha Mayolo ambapo ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Aidha, katika ziara hiyo kamati ilitembelea na kukagua ukamilishaji wa nyumba ya Mkurugenzi na watumishi pamoja na jengo la Utawala.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango walipongeza wasimamizi wa miradi kwa usimamizi wao mzuri na waliagiza uongozi wa Halmashauri kuendelea kuwasimamia mafundi ili waongeze Kasi ya ujenzi na waweze kukamilisha kwa wakati.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda