Katika kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika katika ukumbi wa Malaika siku ya tarehe 23/5/2024, kikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama (CCM), Ndugu Mayaya A. Magesse alisema lengo la kikao hiki ni kwa ajili ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha robo ya tatu 2023/2024.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM, wakiwa kwenye mkutano katika ukumbi wa Malaika
Kamati ya siasa ya Wilaya ilifanya ziara ya siku tatu kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo katika majimbo yote matatu yaliyopo katika Wilaya ya Bunda na kuridhishwa na miradi yote. Pia, walimpongeza Mh. Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dkt Vicent Anney kwa ufuatiliaji na usimamizi katika miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mh. Dkt. Vicent Anney
Aidha, katika kikao hicho Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi aliwatunuku vyeti vya pongezi watumishi watatu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kuweza kusimamia na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi kwa ufanisi katika miradi mbalimbali.
Watumishi waliotunukiwa vyeti hivyo vya pongezi ni Muhandisi wa Halmashauri Ndugu Timothy Mwanjala, kwa usimamizi wake mzuri wa miradi yote ya ujenzi inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Timothy Mwanjala, Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda
Ndugu Johaness Bucha, Mratibu Mkuu na Msimamizi wa miradi ya kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, na Ndugu Roberth Nsemba ambaye ni Mwalimu kwa usimamizi wake mzuri katika ujenzi wa nyumba za watumishi Tirina, ambapo cheti chake kilipokelewa na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Bi. Nambua Semlugu.
Ndugu. Johanes Bucha, Mratibu na Msimamizi Mkuu wa miradi ya kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Dkt Vicent Anney alisema Serikali ya awamu ya sita imetekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za Afya, Elimu, Kilimo,uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, miundombinu ya barabara, maji, usalama wa raia, uhifadhi maliasili na utulivu wa kisiasa.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda