• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WA KATA YA NYAMUSWA NA KETARE KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI YA ZIWA VIKTORIA, KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA.

Posted on: January 6th, 2025

Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA), siku ya  tarehe 06/01/2025 imetambulisha mradi wa maji kutoka Butiama hadi Nyamuswa, kwa wananchi  wa Kata za Nyamuswa na Ketare, zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya  Bunda.

BUWSSA imetambulisha mradi huo kwenye mkutano  wa hadhara ulioandaliwa  na Mbunge wa Jimbo la Bunda Mh. Boniphace Getere, wakati alipokuwa akisikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa Kata ya Nyamuswa.

Mkurugenzi Mtendaji wa BUWSSA,  Bi. Esther Gilyoma amesema Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya maji inatekeleza mradi wa kusambaza maji kupitia chanzo cha maji ya ziwa Viktoria.

" Utekelezaji wa mradi huo, unatarajia kuanza tarehe 01/02/2025 na kukamilika tarehe 30/01/2026, kwa gharama ya Tshs Bill 8.3 fedha kutoka Serikali kuu na  utatekelezwa na Wakandarasi wawili ambao ni MOLI OIL MILLS pamoja, na GAT ENGINEERING CO. LIMITED". Alisema Bi. Gilyoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa BUWSSA amesema,  vijiji vitakavyo nufaika na mradi huo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ni vijiji vitano (5), ambavyo ni kijiji cha Bukama, Makongo A, Makongoro B, Nyamuswa na Tiring'ati.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Stafa Nashoni, aliwashukuru na kuwapongeza BUWSSA katika usimamizi wa mradi huo na aliahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha wanatekeleza na kuukamilisha mradi huo kwa wakati ili wananchi wa Nyamuswa na Ketare waweze kupata maji safi na salama.

Pia, alimshukuru na kumpongeza Mh. Getere kwa kuandaa na kufanya mkutano wa hadhara kwa wananchi wa Jimbo la Bunda akiwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi wake.

Aidha, Ndugu Nashoni alimpongeza na kumshukuru Mh. Mbunge kwa kuweza kusimamia na kuhakikisha mradi huu wa maji kutoka Ziwa Viktoria unaletwa katika Kata za Nyamuswa na Ketare, ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.

Mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kupitia Wilaya ya Butiama hadi Nyamuswa unasimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA), chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa BUWSSA.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA MPANGO MKAKATI

    April 25, 2025
  • PROJECT ZAWADI YAIPIGA TAFU MASHINDANO YA UMITASHUMTA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

    April 07, 2025
  • WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA TUZO NA ZAWADI .

    April 03, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika: 0742163056

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda