Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mwibara na Bunda Bw. Amos Kusaja amemtangaza Mhe Mwita Getere wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda na Mhe Charles Kajege wa Chama cha Mapinduzi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mwibara baaada ya kushinda Uchaguzi mkuu wa Mwaka2020,uliofanyika siku ya Jumatano 28Oktoba,2020.
Akitangaza matokeo hayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw. Kusaja amesema jumla ya vyama vilivoshiriki kwenye uchaguzi mkuu ni vitatu kwa majimbo yote mawili Mwibara (CCM,SAU na CHADEMA) na Jimbo Bunda CCM, CHADEMA na NCCR.
Akisoma matoke hayo Bw. Kusaja amesema mgombea wa chama cha SAU Katika Jimbo la Mwibara Nyombo Mtani amepata kura 506,CHADEMA Vedastus Mahendeka kura 10571 na Charles kajege wa CCM amepata kura 19,770 na Katika Jimbo la Bunda amemtaja Coanel Agust(NCCR)amepata kura245 ,Samwel Ndalo (CHADEMA)amepata kura 5596 na Mwita Getere wa CCM amepata kura 14203.
“Katika Jimbo la Mwibara idadi ya watu waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura walikua ni 70,496 idadi halisi ya waliopiga30,847 kura zilizokataliwa 985na zilizoharibika na Jimbo la Bunda idadi ya watu waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura walikua ni 47585 idadi halisi ya waliopiga kura 20709 kura zilizokataliwa 665”.Alisema Kusaja
Aidha Msimamizi wa Uchaguzi Bw.Kusaja aliwakabidhi Hati ya Ubunge Bw.Mwita Getere Wa Jimbo la Bunda na Charles Kajege wa Jimbo la Mwibara,kama Wabunge halali wa majibo hayo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda