Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Joshua Nassari ametilia mkazo wa kuongeza tija ya uhamasishaji wa kilimo cha zao la pamba ili kuongeza tija katika zao hilo.
Mhe Nassri amesema hayo katika kikao cha uhamasishaji wa kilimo cha zao la pamba kilichofanya Novemba 16, 2021 katika ukumbi wa Malaika.
Mhe Nassari amesema kuwa ni wajibu wa viongozi wa Wilaya ya Bunda kusimamia kwa ukaribu shughuli za kilimo cha pamba ili kufanikisha malengo ya Wilaya kuzalisha Tani 50,000 katika msimu ujao wa zao la pamba.
‘’Wataalam wa kilimo na viongozi wote mkasimamie ipasavyo ili kuweza kufikia lengo la Wilaya kuzalisha tani 50,000 na kuongeza tija katika zao hili’’alisema Mhe Nassari
Aidha Mhe.Nassari ametoa shukrani kwa balozi wa pamba Bwa.Aggrey Mwanri kwa kutoa mafunzo kwa Wataalam na Wakulima wa Bunda.
‘Nina imani kupitia mafunzo haya,Bunda tutafanya vizuri zaidi’’.alisema Mhe. Nassari
Kwa upande wake, Balozi wa zao la pamba Bwa.Aggrey Mwanri amesema kuwa kilimo cha zao la pamba kinahitaji usimamizi na kufuata kanuni bora ,ambazo zitamuwezesha mkulima kuzalisha kwa tija.
‘’kwa kuzingatia matumizi ya mbolea,mbegu bora,kufuata vipimo vilivyopendekezwa na wataalam itasiadia kufikia malengo ya Wilaya,Mkoa na kitaifa katika zao la pamba’’alisema Bwa. Mwanri
Aidha Bwa. Mwanri ameeleza zaidi kuwa kilimo cha pamba kinaweza kubadilisha maisha ya Wananchi wa Bunda kiuchumi kama kutakua na mkakati madhubuti wa uzalishaji wenye tija.
‘Juhudi ziongezeke baada ya mafunzo haya ili kuvuna zaidi katika zao la pamba’.alisema Bwa.Mwanri
Awali bwa.Mwanri alitaja kanuni mpya katika zao la pamba ni sentimita 60 mstari kwa mstari na sentimita 30 mche hadi mche lengo ikiwa kuzalisha kilo 300 hadi 1000 kwa hekari moja.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi.Changwa Mkwazu ametoa shukrani kwa balozi wa Pamba Bwa.Aggrey Mwanri kwakutoa elimu mpya juu ya uzalishaji pamba.
‘Awali wakulima walikua wanapata wastani wa kilo 300 badala ya 1000 ,kupitia mafunzo haya tunategemea mabadiliko makubwa’.alisema Bi Mkwazu
Aidha Bi.Mkwazu ameahidi kushirikiana na Wataalam wa kilimo, watendaji wa vijiji na viongozi wengine katika hatua ya upandaji,umwagiliaji wa dawa mpaka uvunaji.
‘ili kuhakikisha tunapata pamba iliyo bora na inayokubalika katika soko’’alisema Bi.Mkwazu
Kampeni ya kuongeza tija ya uzalishaji wa kilimo cha zao la pamba itaendelea kufanyika ngazi ya vijiji na mtaa ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda itafanyika katika vijiji 78 na Halmashauri ya mji wa Bunda Mitaa 21.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda