Mkuu wa wilaya ya Bunda Mh: Lydia Bupilipili amefanya kikao na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Bunda Januari29,2020.
Akizungumza katika ukumbi wa Shule ya Msingi Kibara B, Mh Bupilipili aliwapongeza Watumishi kwakuweza kutekeleza agizo la Mh: Rais lakutaka kila Halmashauri kuhamia katika Eneo la kiutawala,
Pia mh Bupilipili aliwataka Watumishi kubainisha changamoto wanazokutana nazo kwa kipindi hichi walichohamia Katika Eneo la utawala.
Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bunda Bwa.Amos Kusaja alisema Watumishi wote wamepata vyumba vya ofisi hapa Kibara,ni Ofisi chache ambazo bado wanafanya majukumu yao mengine pale Ofisi za zamani na hii kutokana mifumo bado haijahamia na kazi nyingi zinategemea mifumo.Mpaka sasa niwapongeze Watumishi kwakujituma kwa kipindi hiki cha uwahamisho.Watumishi hawa wanatumia garama zao binafsi Ofisi haijawalipa stahiki zao za uhamisho lakini pia utaratibu unafanyika kwaajili yakuwapatia stahiki zao .alisema Mkurugenzi Mtendaji.
"Taratibu za uhamishaji wa mifumo unaendelea kufanyika ili huduma zote ziwenipatikana huku".
Kwa upande wa Watumishi walibainisha changamoto wanazokutana nazo katika eneo la utawala ikiwemo vyumba kupanda bei, miundombinu hairidhishi ikiwemo vyoo na barabara kuwa mbovu, changamoto ya maji, kupanda bei bidhaa mbalimbali na vyumba vyingi kutokuwa na hadhi na usiri kwa Watumishi na wananchi kuwarushia mawe watumishi.
"Nyumba ya Mtumishi na Mtu wa kawaida havioneshi tofauti hivyo tunashauri Mh Mkuu wa Wilaya utusaidie kuongea na Wananchi wapunguze bei na kuwahamasisha kujenga Nyumba Bora"
Changamoto nyingine kubwa ni kuhusu stoo ya chanjo,kwa kawaida stoo ya chanjo inatakiwa kuwa na vyumba vitatu,ikiwemo chumba cha majokofu takribani Saba,chumba cha kutunzia mabox ya silinji na vifaa vingine vikavu na chumba cha ofisi ambapo kwa hapa Kibara hatujapata jengo litakalokidhi mahitaji hayo.pamoja na hivo pia inahitajika uwepo wa standby generator ikitokea dharula ya umeme kukatika.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ilihamia rasmi katika Eneo lake lakiutawala mnamo oktoba28,2019 ikiwa niutekelezaji wa agizo la muheshimiwa Rais Mh: Dkt John Pombe Magufuli lakuagiza kila Halmashauriya kuhamia katika Eneo lake kiutawala.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda