Mkuu mpya wa Mkoa wa Mara Ndg. Adamu Malima ameingia rasmi Mkoani Mara akitokea Jijini Mwanza na kupita Wilayani Bunda kwa lengo la kujitambulisha kwa Wadau mbalimbali wilayani hapa. Pamoja na utambulisho huo, mkuu huyo wa mkoa wa Mara aliweza pia kugusia masuala kadhaa ambayo atayasimamia mara atakapoanza kazi rasmi.
Baadhi ya maeneo aliyogusia kama vipaumbele ni pamoja na Amani na usalama wa raia, Ukuaji wa Uchumi hasa katika kuleta maendeleo ya Wananchi na Uboreshaji wa Huduma za Jamii. Mkuu huyo wa Mkoa wa Mara alisisitiza kuwa ni vyema kila sekta ijitathmini kwa kufanya utafiti juu ya namna itakavyoshiriki katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Wananchi wa Wilaya ya Bunda.
Waliohudhuria katika kikao hicho cha utambulisho ni pamoja na Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala (W), Wakurugenzi Watendaji wa Mji na Wilaya, Maafisa Tarafa, Wakuu wa Idara na Vitengo wa pande zote mbili, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya. Mkuu huyo wa Mkoa aliendelea na safari yake ya utambulisho katika Wilaya zingine za Mkoa wa Mara
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda