Mkuu wa Mara Mhe.Ally Hapi amewapongeza wanakijiji cha Isanju Kata ya Iramba kwa kutoa eneo la ukubwa wa takribani Hekari 40 kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika kijiji hicho.
Pongezi hizo zimetolewa wakati alipotembelea eneo hilo la ujenzi wa Kituo Afya 13Oktoba 2021.
Mhè Hapi amesema kuwa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan alijua kuwa hapa mlianza kuhangaika na ujenzi wa zanati hivyo ikatolewa milioni 250 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha kisasa chenye uwezo wa kufanya upasuaji na huduma nyinginge kubwa.
“Kina Mama wajawazito operesheni zote zitafanyika Isanju''Alisema Mhe.Hapi
Aidha Mhe Hapi alitoa rai Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya kuhakikisha ujenzi unaanza haraka iwezekanavyo.
“Nisingependa kuona watu wanakaa na pesa wakati Raisa ameshazitoa,Nisingependa kuona ucheleweshwaji wa mradi huu”Alisema Mhe Hapi
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri DR.Nuru Yunge lengo Mradi ni kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi wa Iramba ambao kwa sasa wanatumia kituo cha Afya cha Kasahunga kwa huduma za rufaa kilometa 33 kutoka kijiji cha Isanju.
“Tunaamini kituo hiki kikikamilika wananchi hawatopata usumbufu wa huduma za rufaa".alisema Dr.Yunge
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Isanju Bwa. Zakayo Kabwe amesema kuwa Wananchi wa Isanju wameshiriki asalimia mia katika upatikanaji wa eneo.
“Natupo tayari kushiriki katika ujenzi"alisema Kabwe
Bwa.Kabwe alitoa shukrani kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Samia Suluhu Hassan kwakutoa fedha kwaajili ya kusambaza maji kijiji cha Isanju pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya.
“Tunashukuru"alisema Bwa.Kabwe
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ilipokea fedha Tshs.250,000,000 tarehe 29/9/2021 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya kijiji cha Isanju kata ya Iramba ,Halmashauri pia inatarajia kuanza ujenzi mara tu baada kupata maelekezo kutokq OR-TAMISEMI.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda