Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mhe. Charles Manumbu amewataka Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kusimamia mapato pamoja na miradi ya maendeleo ili kufanikisha lengo la serikali kuweka miundombinu bora kwa wananchi.
Akizungumza katika Mkutano wa baraza la Madiwani robo ya nne 2020/2021 lilifanyika Septemba 23 katika ukumbi wa Kanisa la Kibara .Mhe Manumbu amesema kuwa ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha mapato yanakusanywa na kupeleka fedha benki kwa wakati ili kuepusha matumizi ya fedha mbichi.
‘’sisi kama madiwani tutasimamia kwa nafasi zetu niwakumbushe wataalam kusimamia mapato kwa uwaminifu ili kuepusha kutengeneza mazingira ya rushwa’’.amesema mhe.Manumbu
Aidha Mhe. Manumbu amewataka wataalamu kusimamia miradi ya maendeleo ipasavyo kwakuhakikisha taratibu za manunuzi zinafuatwa pamoja na kufuatilia hatua za ujenzi ili kuhakikisha ubora wa majengo unapatikana.
‘’Wataalamu wamajengo na manunuzi niwajibu wenu kusimamia miradi yote katika hatua ya awali mpaka mwisho ili kupata majengo yaliyo bora’’.amesema Mhe.Manumbu
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bunda Bi Changwa Mkwazu amesisitiza katika kusimamia mapato pamoja na miradi ya maendeleo ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe Samia Suluhu Hassani.
‘’Halmasahauri yetu ina vyanzo vingi vya mapato niahidi tu mimi na wataalamu wangu tutasimamia ipasavyo kuhakikisaha tunasonga mbele katika ukusanyaji mapato na kusimamia miradi’’amesema Bi Mkwazu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Joshua Nassari ametoa pongezi kwa Waheshimiwa Madiwani kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kudhamilia kuziba mianya inayo hatarisha kupoteza kwa mapato.
‘’nitoe rai kwa wataalamu kutoa ushirikiano kwa madiwani katika kusimamia mapato yasipotee’’amesema nassari
Kwahatua ingine baraza limeazimia kusimamisha kazi watumishi 11 ili kupisha uchunguzi watuhuma zinazowakabili katika upande wa manunuzi,mapato na ujenzi wa miradi ya maendeleo katika ngazi ya kijiji mpaka Halmashauri na watumishi watatu kupewa onyo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda