Wananchi wa Kijiji cha Kurusanga Kata ya Salama iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Bunda, wameombwa kuendelea kuchukia uhalifu na kujizuia kujichukulia sheria mkononi kwani inasababisha madhara hata kwa wasio na hatia.
Rai hiyo, imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ndg Pius Lutumo, siku ya tarehe 8/1/2025 ,alipofanya ziara katika Kata ya Salama ili kuongea na wananchi juu ya masuala ya ulinzi na usalama.
Ziara hii imekuja baada ya kutokea tukio la mtu mmoja alieshukiwa kuwa ni mwizi wa Ng’ombe kupigwa na kuuwawa na wananchi wenye hasira kali katika Kijiji cha Kurusanga siku chache zilizopita.
Pamoja na hayo, Kamanda ameendelea kwa kusema kua matatizo haya ya mauaji,wizi na ukorofi huwa yanaanza na uzembe wa wananchi kwa nafasi zao kutochukua hatua stahiki kila mara pale tatizo linapojitokeza hali inayosababisha hali ya kulea tatizo.
Hivyo, ameagiza Kata kuunda kamati za ulinzi na usalama kuanzia ngazi za vitongoji na vikundi vya ulinzi ambavyo vitajengewa uwezo na ofisi ya OCD.
Kamanda Lutumo alitoa kauli ya kuwataka wale wote waliokimbia miji yao kutokana na tukio la mshukiwa wa wizi kuuwawa warudi mara moja kwenye miji yao wakati huu ambapo jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wake kwani Serikali ina mkono mrefu na haijashindwa kuwapata.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda