Wakala wa Maji Usafi wa mazingira Vijijini imefanya mkutano wa Mwaka wa Pilli wa Sekt na Wadau wa Maji na Usafi wa mazingira 28Agosti,2020 katika ukumbi wa Malaika uliopo Bunda Mji, lengo la majadiliano ni kuwa nauelewa wa pamoja kuhusu maendeleo ya Sekta ya Maji katika Wilaya ya Bunda kwa ujumla.
Akifungua Mkutano huo mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Lydia Bupilipili amesema anawapongeza Wizara ya Maji kupitia RUWASA Ngazi ya Mkoa na Wilaya kwa kuweka utaratibu wa kuwepo kwa mkutano wa wadau ambapo unasaidia kutambua wapi tulipo toka,wapi tulipo na wapi tunakwenda na hii ni chachu ya maendeleo kwa jamii inayotunguka kwakuweza kutatua changamoto za maji kwa jamii kupitia vikao hivi.
“utaratibu wa vikao vya wadau wa maji ni muhimu husaidia kutambua changamoto mbalimbali na hata kujua nani anakwamisha katika kuleta maendeleo kwa jamii kupitia maazimio ya yanatolewa katika kikao”.alisema Mhe Bupilpili
Mhe Bupilipili amesema kuwa huduma ya maji katika maisha ya Mwanadamu halikwepeki, uwepo wa maji ya uhakika katika jamii husaidia kufanya Wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ya jamii, hivyo ni muhimu kila mmoja wetu kuwajibika kwa nafasi yake ili kuondoa na kuimaliza changamoto ya maji katika jamii.
“kama serikali ni jukumu letu kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama”.
Aidha Bupilipili ametoa wito kwa viongozi wa serikali ya vijiji kutobadilisha matumizi ya fedha za miradi ya maji kupeleka katika miradi mengine kwani kufanya hivo ni kuendelea kufanya akina mama wateseke kufuata maji umbali mrefu.
“kila kiongozi ni jukumu lake kuleta hamasa kwa wananchi kushiriki katika miradi ya maendeleo itasaidia kutobadilisha matumzi ya pesa za miradi ya maji kutumika katika miradi mengine”.
Naye Kaimu Meneja RUWASA Bunda Eng. Lucas N.Madaha amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha Bilioni 1.3 za kutekeleza miradi ya maji ambayo itachangia kuondoa na kupunguza changamoto ya maji.katika maeneo mbalimba hapa Bunda.
“Fedha hizi zimeletwa na serikali kwaajili ya Wananchi wake ili wasipate tabu kutembea umbali mrefu wa kufuata maji hasa akina mama”.alisisitiza Eng.Madaha
Aidha Eng Madaha amesema kuwa Serikali inafanya mengi katika kuhakikisha kuwa inapata maji katika vyanzo vilivyoboreshwa jumla ya shiilingi Bilioni 6 zimeekezwa katika kipindi cha Serikali ya awamu tano chini Dkt John pombe Magufuli katika kuboresha huduma ya maji.
“Hivyo wadau wa maji ni muhimu kuelewa uchangiaji na kulinda miundombinu ya huduma ya maji ili iwe endelevu”.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ni moja kati ya Halmashauri 87 zilizonufaika na mradi wa maendeleo endelevu ya Maji vijijini(Rural Water Supply and Sanitation Program) ikiwa huduma ya maji imeongezeka kutoka asilimia 43.5 mpaka asilimia 68.9 .
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda