Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Stafa Nashoni, ambaye ni mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi, siku ya tarehe 14/2/2025 alifungua mkutano wa baraza hilo kwa kuwashukuru wajumbe kwa kuweza kuhudhuria katika mkutano huo ambapo alisema lengo la mkutano huu ni kujadili na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Dicksoni Balige aliwasilisha rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi ili iweze kujadiliwa na kupitishwa katika baraza hilo kabla ya kuanza utekelezaji wake.
Wajumbe wa baraza walipokea na kuipongeza Halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa rasimu nzuri ya mpango na bajeti waliyoiwasilisha, ambapo walisema imezingatia maslahi ya watumishi pamoja na kuweka malengo Madhubuti katika kuhakikisha Halmashauri inaongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka katika vyanzo vyake vyote.
Baraza la wafanyakazi liliridhia na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti, ambapo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri inatarajia kukusanya kiasi cha Tshs Billioni 36,516,498,215/=
Naye, Katibu wa TALGWU mkoa wa Mara Ndugu Mussa Mashamba aliwataka watumishi kuwa na umoja na ushirikiano katika utendaji wao wa kazi kwa kuhakikisha wanapendana.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda