Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Kusaya ambaye alimuawakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi katika maonesho ya Mkoa ya utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni yaliyofanyika katika Wilaya ya Rorya siku ya tarehe 8/11/2024.
Ndugu Kusaya alisema, Leo hii nipo hapa kwa ajili ya kushuhudia maonesho haya ya utoaji wa huduma na lishe shuleni ambapo nimeweza kutembelea na kukagua Stoo ya kuhifadhia chakula shuleni, bustani za mbogamboga na shamba la shule, pia nimeweza kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali yaliyopa uwanjani hapa ambapo nimeweza kupata elimu ya lishe na kuona namna gani Halmashauri zetu zinazingatia utoaji wa chakula na lishe kwa wanafunzi wa shule zetu.
" Bado tunachangamoto katika utoaji wa chakula shuleni kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa jumla ya shule za msingi 190 na shule 6 za Sekondari hazitoi kabisa chakula shuleni, ambapo 52% ya shule za msingi ndizo zinatoa chakula na 54%kwa shule za Sekondari zinatoa chakula, hivyo tunalo jukumu kubwa kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha wazazi, jamii na wadau kuendelea kuchangia chakula shuleni." Alisema.
Ndugu Kusaya alisema tumekuwa tukishirikiana na wadau mbalimbali katika kuhamasisha utoaji wa huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni hivyo kupelekea Mkoa wetu wa Mara kuwa wa kwanza katika uanzishwa wa muongozo wa utoaji wa chakula shuleni ambapo, muongozo huo ulianzishwa kutokana na kuwepo wa mradi uliokuwa unahamasisha utoaji wa chakula shuleni uliojulikana kwa jina la " Chakula kwa Elimu" na ulitekelezwa na shirika la " Project Concerning International" kuanzia mwaka 2011 hadi 2020, hivyo Mkoa wetu wa Mara unapaswa kujisifu kuwa Mkoa wa kwanza kwa utoaji wa chakula shuleni.
" Nitoe wito kwa wenzetu wadau wanaopenda kutusaidia katika utoaji wa huduma ya chakula shuleni kuhakikisha wananunua chakula ndani ya nchi na sio kutuletea kutoka nje ya nchi" Alisema.
Ndugu Kusaya alisema lengo la Mkuu wa Mkoa wa Mara ni kuona shule zote za serikali na binafsi, za msingi na Sekondari zinatoa chakula ifikapo Januari, 2025.
Hata hivyo vyeti vya heshima vilitolewa kwa shule zinazo toa chakula kwa wanafunzi kwa asilimia miamoja(100%).
“Utoaji wa Chakula shuleni ni jambo la lazima,pamoja tuwalishe watoto wetu”
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda