Wilaya ya Bunda imeadhimisha maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii siku ya tarehe 8/12/2024.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndugu Salum Khalfan Mtelela, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh.Dkt Vicenty Anney, ameongoza kamati ya usalama ya Wilaya, wakuu wa taasisi zilizopo Wilaya ya Bunda, wakuu wa idara na vitengo kutoka Halmashauri zote mbili, pamoja na Wananchi wa Wilaya ya Bunda, katika zoezi la upandaji miti, ambapo miti 500 ya kivuli na matunda ilipandwa katika eneo la Magereza lililopo Bunda Mjini, pia, walishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bunda.
Mbali na zoezi la upandaji miti na kufanya usafi, pia,kulikuwa na michezo mbalimbali ambayo ilishirikisha wananchi na watumishi wote wa Wilaya ya Bunda.
Michezo mbalimbali ilichezwa ambayo ni mpira wa miguu kwa watumishi wa Wilaya ya Bunda, kukimbiza kuku, kutembea na yai mdomoni, mchezo wa draft, mashindano ya kunywa soda na mingine mingi.
Katika bonanza hilo zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washiriki walioshinda katika michezo, na zawadi hizo zilitolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndugu Salum Khalfan Mtelela.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda