Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu. Oscar Jeremiah Nchemwa siku ya tarehe 20/1/2025 ameongoza kikao cha tathimini ya shughuli za lishe kwa kipindi cha robo ya pili kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba,2024.
Aidha Ndugu, Nchemwa amemuagiza Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kusimamia na kuhakikisha vijiji vyote vinatunga sheria za lishe ili kuwahimiza wananchi kushiriki katika kuchangia chakula shuleni.
Naye, Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bi.Saumu Abdallah aliwasilisha kadi alama kwa ngazi ya Halmashauri, Kata na Chama kwa kipindi cha robo ya pili, na aliomba na kushauri jitihada ziongezeke zaidi katika uhamasishaji wa kuchangia chakula ili kuhakikisha wanafunzi wengi wanapata huduma ya lishe shuleni kwa kutoa elimu na kuonyesha athari za watoto kutopata lishe shuleni, ambazo zinapelekea kushuka kwa ufaulu.
“Kuna shule nyingi zinazotoa huduma ya chakula shuleni lakini ni watoto wachache wanao pata huduma hiyo”.amesema Bi.Saumu
Kwa upande wake, Mkuu wa divisheni ya Afya,ustawi wa jamii na lishe,ambaye ni katibu wa kikao cha lishe, Dkt.Hamidu Adinani alimuomba Mkurugenzi Mtendaji kutoa kipaumbele katika masuala ya lishe ili kiweze kutimiza shughuli za lishe kama zilivyo pangwa, pia, aliomba divisheni na vitengo mtambuka vinavyo shughulika na masuala ya lishe shuleni na kwenye jamii kutenga bajeti ambazo zitasaidia katika utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kila robo kwa mwaka mzima.
Hata hivyo, wajumbe waliazimia shule zote za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kutenga mashamba kwa ajili ya kilimo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda