Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu Noel Shamazugu siku ya tarehe 13/2/2025 amefungua mkutano wa baraza la Wafanyakazi kwa kuwashukuru wajumbe wote waliohudhuria, pamoja na vyama vya Wafanyakazi waliofika kwa ajili ya uzinduzi wa baraza jipya la wafanyakazi.
Ndugu Shamazugu alisema, leo hii tupo hapa kwa mambo mawili muhimu ambapo jambo la kwanza tutachagua viongozi wapya ambao ni Katibu na Katibu msaidizi katika kusimamia na kuongoza baraza hili kwa kipindi cha miaka mitatu na pia, tutafanya uzinduzi wa baraza jipya baada ya kupata viongozi wapya.
Afisa Kazi wa mkoa wa Mara Ndugu Perfectus Kimaty aliongoza uchaguzi wa viongozi hao kwa kuwataka wajumbe kuweza kupiga kura ili waweze kuwachagua viongozi hao wapya na alisema uchaguzi huu ni wa haki kila mjumbe atapiga kura ya siri kulingana na majina ya watumishi wawili yaliyopendekezwa ambapo alisema, yule atakayeongoza kwa kura ndio atakuwa Katibu na alibaki atakuwa Katibu Msaidizi kama muongozo na kanuni za baraza la wafanyakazi inavosema.
Wajumbe waliopiga kura za siri walikuwa 54 na hakuna kura hata moja iliyoharibika, hivyo kumtangaza Bi. Pili Masaza kuwa Katibu wa baraza la wafanyakazi kwa kura 39 dhidi ya Amos Kaunya aliyepata kura pungufu hivyo, kupelekea Bi. Pili Masaza kutangazwa kuwa Katibu na Amosi kuwa Katibu msaidizi wa baraza la wafanyakazi, ambapo wataongoza baraza kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Afisa Kazi aliwashukuru wajumbe wote walioshiriki katika kupiga kura za siri na kuweza kuwachagua viongozi hao wapya ambao wataongoza baraza la wafanyakazi.
"Baraza hili ni chombo muhimu cha kushauri Halmashauri kuhusu masuala mbalimbali ya maslahi ya wafanyakazi na upangaji mipango na utekelezaji wake kwa ujuml ." Alisema Ndugu Kimaty.
Ndugu Kimaty aliwafundisha wajumbe kufahamu muongozo,kanuni, sheria na taratibu za baraza la wafanyakazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kusema, kwamba lengo kuu la kuwa na baraza la wafanyakazi katika Halmashauri ni kwa ajili ya kumsaidia muajiri katika kutambua haki za mfanyakazi wake, na pia kumtetea mfanyakazi na maslahi yake kwa kuhakikisha anapata haki zake za utumishi anapokuwa kazini kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za kazi.
Aidha, amewataka wajumbe kuhakikisha wanashiriki kikamilifu bila hofu kwa kutumia fursa hiyo muhimu kujadili hoja zinazojitokeza ili kukamilisha shughuli za baraza. Kwa upande wao viongozi waliochaguliwa wamewashukuru wajumbe kwa kuwaamini na kuwapa dhamana ya kuwaongoza huku wakiwaahidi kuwatumikia kwa kufata sheria, kanuni na taratibu za baraza la wafanyakazi.
Baraza la wafanyakazi ni baraza ambalo lipo kwa mujibu wa agizo la Rais Na.1 la mwaka 1970 ambalo lina lengo la kuwashirikisha wafanyakazi wa ngazi zote katika utekelezaji wa shughuli za taasisi kwa kushirikiana na uongozi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda