Kupitia mradi wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi (BCRAP) siku ya tarehe 17/12/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imepokea jumla ya mizinga 90 ya kufugia nyuki,pamoja na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuvuna asali.
Mapokezi hayo yamefanyika katika Ofisi za Kasahunga, ambapo mratibu anayesimamia mradi Ndugu Johanes Bucha alisema vifaa hivyo pamoja na mizinga vitagawiwa kwa vikundi vya Ufugaji nyuki ambavyo ni wanufaika wa mradi wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Ndugu Bucha alisema Mizinga pamoja na vifaa hivyo vimegharimu kiasi cha Tsh Milioni 23,932,000/= na wanatarajia kuwapatia wanufaika wa mradi wa vikundi vya ufugaji nyuki ambao walishapewa mafunzo.
Mradi wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi ni mradi unaosimamiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ukidhaminiwa na kufadhiliwa na Baraza la Mazingira Tanzania (NEMC), wakishirikiana na Mfuko wa Mazingira Duniani (Adaptation Fund).
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda