• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Halmashauri ya Wilaya Bunda yaadhimisha siku ya wazee Duniani kwa kugawa Kadi 593 kwa Kata ya Chitengule na Kata ya Nansimo.

Posted on: October 2nd, 2020

Halmashauri ya Wilaya ya Bunda  imeadhimisha siku ya wazee Duniani iliyombatana na kauli mbiu isemayo “Familia na jamii tuwajibike kuwatunza Wazee”.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika  Kijiji cha Nansimo Kata ya Nansimo yakiambatana na ugawaji wa kadi 593 za msamaha wa matibabu ikiwa  kadi 323 ni  kata  ya Nansimo  na 270 kata ya Chitengule , ipamoja na utoaji wa huduma za Afya kama vile upimaji,ushauri,Dawa na Rufaa.

Akizungumza  mgeni rasmi kwa niaba ya  Mkurugenzi Mtendaji Bwa.Oscar Jeremia amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa Wazee hasa katika kuleta maendeleo ya Taifa letu  hivyo katika kuadhimisha siku hii ni moja wapo ya kuthamini mchango wenu.

“wazee mmefanya  kazi kubwa sana ndio maana serikali inawaenzi”.

Katika Kuadhimisha Siku ya Wazee,Bw.Jeremiah amesema ipo mikakati madhubuti imeandaliwa na  Halmashuri ili  kuhakikisha haki za Wazee zinapatikana kwa wakati.

Ameitaja mikakati hiyo kuwa ni kuunganisha wazee wasiojiweza na Mfuko wa TASAF na Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF),kuwatembelea Wazee na kufanya Mikutano ili kuwasikiliza , kuunganisha na vikundi ili kupata mkopo  ya 2% ya Halmashauri,kupinga na kuzuia kiwango kikubwa cha mauaji ya Wazee kwa tuhuma za uchawi ,kuwatambuana na kuhakikisha wazee wote wenye umri wa miaka 60 na kuendelea wanapata vitambulisho vya msamaha wa matibabu.

Aidha Bw.Jeremiah alitoa wito kwa  familia  na Jamii kuendelea kutunza Wazee ili wasipate upweke.

“Tusiwakimbie wazee maana wao ndo wametukuza mpaka tulipofika”.alisisitiza  Jeremiah

Naye Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri  Bi Fausta Parali amesema tunapoadhimisha siku ya wazee sio tunakutana tu bali tunapata nafasi yakutambua changamoto mbalinbali zinazowakabili wazee.

Bi. Parali amesema pia kuwa Halmashauri kupitia kitengo cha Ustawi wa Jamii inashughulikia kuwaunganisha  wazee na family zao wanapotelekezwa au kutupiwa mzigo wa wajukuu.

“Kila mzee anae achiwa wajukuu na ikiwa wazazi wa mtoto yupo inabidi apatiwe huduma na mzazi wa mtoto huyo”alisisitiza Parali

Katika hatua nyingine muwakilishi wa Wazee Bwa.Asaf Mkama ameishukuru serikali ya awamu ya Tano kwakuendelea kuwa tunza na kuthamini mchango wao.

“Nimefarijika kuona viongozi wetu wanatukutanisha wazee kama sisi kutoa mawazo yetu

Aidha Bwa. Mkama ameiomba serikali kuwapatia miradi mbalimbali kama mashine ya kusaga unga ili waweze kujikomboa kiuchumi na kukidhi mahitaji.

“Tunaomba serikali itupatie miradi itakayo tusaidia kuinua kipato”alisema Mzee Mkama.

Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Mabaraza ya Wazee  ya Kata ya Chitengule na Nansimo  ikiwa jumla ya Wazee 9,994 wametambuliwa katika vijiji 78 na ka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI SALAMA December 17, 2020
  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWIBARA December 17, 2020
  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI CHITENGULE December 17, 2020
  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MURANDA December 17, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Shule za Msingi,Mugeta,Sanzate na Nyamitwebili zilipo Halmashauri Wilaya ya Bunda yanafuika na jengo la Maktaba yaliyofadhiliwa na Shirika lisilo la Serikali PCI

    December 19, 2020
  • Halmashauri Ya Wilaya ya Bunda ya Zindua Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani.

    December 17, 2020
  • Halmashauri ya Wilaya ya Bunda,Butiama ,Serengeti na Musoma Dc yanufaika na Mafunzo ya TARI

    December 05, 2020
  • Halmashauri ya Wilaya ya Bunda yaadhimisha siku ya Ukimwi Duniani.

    December 04, 2020
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2020 Bundadc
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019
  • Sekretarieti ya Ajira
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Mara Secretariet

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kilimani Street

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0677002976

    Hamishika: 0783669938

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda